Tuesday, June 7, 2011

Shona gauni au suruali kulingana na ukubwa wa kitambaa chako

Shona suruali au gauni lako kulingana na ukubwa wa kitambaa chako. Binadamu wengi ni waoga wa kufanya kitu tofauti na mazoea au desturi. Kama wengine wanafanya harusi za milioni 5 kwanini wewe usifanye ya laki tano kama sio elfu hamsini tofauti tu kisha ukasaidia yatima na masikini ? Harusi ni siku moja, msaada wako kwa wanaouhitaji ni thawabu zitakazoendelea hata uhai wako hapa duniani ukikoma.


Tafakari. Fikiri. Zingatia. Badilika na wasaidie wengine kubadilika. Usiwe mwoga. Badilika. Kuwa tofauti. Na anza kuonesha vipaji na uwezo wako wote katika kuibadili na kuiendelza nchi yako kuanzia leo. Watanzania wasio na elimu, maskini, wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali wanakutegemea wewe. Na malipo yako hayako hapa duniani bali akhera, na siku zetu hapa duniani sio nyingi sana. Usijisahau.

Wewe ni wewe kwanini ujifananishe na wengine ?

TABIA ya kutaka kuishi ili kuwapendeza watu wengine haimsaidii mtu ila tu kwa mambo ambayo ni ya kinidhamu na kimaadili. Uko huru kuishi kama mtu tofauti pamoja na kuishi na kushirikiana na wengine. Usijefanya jambo eti kwa sababu tu wengine nao wanalifanya au walilifanya. Jijue wewe mwenyewe kwanza na kisha ndio uamua njia ya kufuatwa bila kushawishika na watu watakuona vipi au watakusemaje?

Kuwa huru na kuwa tofauti ndio mwanzo wa kuukamilisha ubinadamu na utu wako. Usiwe nyani au kima au sokwe kuiga ya wengine.